
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mwezi Juni umeshuhudia kushuka kwa visa vya utovu wa usalama, kwa mujibu wa Shirika la Kivu Security Tracker linalothathmini hali ya usalama Mashariki mwa nchi hiyo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Visa vya utovu vimeshuka kwa asilimia 19 kwa kipindi cha mwez Juni, katika mikoa ya Ituri, Kivu Kaskazini na Kusini, ambapo kutoka matukio 305 mwezi Mei, visa 247 ndivyo vilivyoripitiwa.
Shirika la Kivu Security Tracker linasema pamoja na kushuka kwa visa hivi, haimanishi kuwa hali ya usalama imeimarika, na kuisisitiza kuwa hali ya raia wa kawaida, inaendelea kuwa mbaya.
Aidha, licha ya kushuka kwa visa vya uhalifu, ripoti ya Shirika hilo inaonesha kuwa waasi wa M23, wanasalia kuwa hatari kubwa hasa kwa usalama wa raia, huku kundi la ADF likiendelea kuchukua maeneo zaidi, ambapo sasa hivi wamefika katika mkoa wa Haut-Uélé.
Katika mwezi huo wa Juni, raia 114 wanaripotiwa kuuawa, na wenhgine 17 kutekwa katika wilaya za Masisi na Rutshuru, wengi wakiwa ni raia wanaodaiwa na waasi wa M23 kuwa wanashirikiana na makundi ya Wazalendo au FDLR.