Iran imethibitisha kupokea mapendekezo na maoni mbalimbali kutoka kwa wapatanishi kadhaa yanayolenga kupunguza mivutano na Marekani, huku Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Esmaeil Baqaei, akisema kuwa Tehran inaendelea na juhudi za kidiplomasia sambamba na hatua zinazochukuliwa na vikosi vya ulinzi vya Iran.

Akizungumza katika mkutano wake wa kila wiki na waandishi wa habari siku ya Jumatatu, Baqaei alijibu swali la Shirika la habari la IRNA kuhusu ripoti za hivi karibuni zinazoashiria kuwa Qatar imewasilisha mipango mipya ya kuhuisha mazungumzo, ikiwa ni pamoja na tetesi kuhusu pendekezo la kusitisha mapigano kwa siku 10 kati ya Tehran na Washington.

Swali hilo pia  lilihusu ziara ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araghchi nchini Qatar kwa ajili ya kutoa rambirambi kwa maafisa wa Qatar kufuatia kifo cha aliyekuwa Amir wa Qatar, Sheikh Hamad bin Khalifa Al Thani; ziara ambayo pia iliripotiwa kuhusisha mkutano wake na mwenzake wa Qatar.

Katika jibu lake Baqaei alieleza kuwa,  ilikuwa wazi kwamba wapatanishi walikuwa wakifanya kazi kikamilifu ili kuzuia hali haliya mambo kuwa mbaya zaidi na wakati huo huo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitaacha jitihada yoyote ya kukomesha uhalifu wa Marekani dhidi ya Iran.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari mjini Tehran, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran aliongeza kwa kusema: Wakati Jeshi la Iran likijibu “kwa nguvu ” na kulenga vyanzo vya uchokozi wa Marekani, mfumo wa kidiplomasia wa Iran pia ulikuwa ukitekeleza majukumu yake kikamilifu.

Esmaeil Baqaei amebainisha kuwa, hati ya makubaliano iliyosainiwa na Iran na Marekani ina vifungu 14 pekee, na kwamba hakuna  kipengele kisichoeleweka vyema. “Maandishi hayo yako wazi kabisa, na Marekani haina sababu yoyote ya kukiuka makubaliano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *