Dar es Salaam. Unakumbuka mizinguo aliofanya Goodluck Gozbert? Yule bishoo aliyeamua kumtumikia Mungu kwa ngoma za kiinjili? Huyo huyo ambaye hata jukwaa la kidunia alipanda kuwakumbusha watu uwepo wa Mungu. Alichoma moto benzi hadharani.  

Benzi alilopewa kama zawadi na Askofu Geor Davie wa Arachuga, akidai lilikuwa na mkosi. Siku hiyo aliondoka na ndinga lake hilo hadi kwenye pori analolijua yeye na kutia kiberiti. Akachukua video na kusambaza mitandano huku akinena kwa lugha.

Hata kama mtu anaamini kitu fulani kina matatizo au hakina baraka. Kuchoma zawadi yenye thamani si suluhisho la busara.  Angeweza kuirudisha kwa yule aliyempa, kuiuza au hata kuitoa kwa mtu mwingine. Mshikaji ni wazi alizingua.

Kuchoma mali ni kitendo cha kukosa hekima na kutothamini kile ulichopewa. Katika maisha na biashara, taswira ni mtaji mkubwa sana. Pindi wanadamu wanapopoteza imani kwa yale maamuzi yako, wanaweza pia kupoteza hamu ya kukuunga mkono kwa mambo mengine.

Msanii, mfanyabiashara au kiongozi hujengwa na kipaji na namna anavyoonekana mbele ya jamii. Kila tendo lina matokeo. Wakati mwingine siyo sheria tu zinazokuadhibu, bali maoni ya watu, kupungua kwa imani yao kwako na kuharibika kwa sifa uliyoijenga kwa miaka mingi.

Ni muhimu pia kutenganisha imani yako na ukweli unaoweza kuthibitishwa. Si rahisi kusema kwa uhakika kuwa tukio fulani ndilo lililosababisha mafanikio ya mtu kutoweka. Mafanikio ya kazi yanaweza kuathiriwa na sababu nyingi tofauti.

Kila mmoja wetu anapaswa kujifunza. Kwamba busara, shukrani na kuheshimu mali. Ni maadili yanayoweza kulinda heshima na taswira yetu kwa muda mrefu. Huwez[ kuchoma mali kibwege. Haya sasa baada ya kuchoma vipi kapaa kisanii au kazimika kisanii? .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *