Azam Media imesaini mkataba wa ushirikiano na waandaaji wa shindano la Miss Universe Tanzania ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuunga mkono majukwaa ya kukuza vipaji vya Watanzania.

Kupitia ushirikiano huo, pande zote mbili zimesema zitatumia jukwaa la shindano hilo kuhamasisha maadili na kuenzi utamaduni wa Kitanzania kupitia maudhui yatakayorushwa kwenye chaneli ya Sinema Zetu ndani ya kisimbuzi cha Azam TV.

Wamesema ushirikiano huo pia unalenga kutoa burudani yenye maadili huku ukiendelea kukuza vipaji na kuwapa fursa washiriki kujitangaza kitaifa na kimataifa.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *