Mbunifu Laineli Ngailo kutoka Kijiji cha Lugenge mkoani Njombe ameendelea kuwa mfano wa ubunifu wa ndani baada ya kufanikiwa kuwasha taa katika baadhi ya kaya za kijiji chake kwa kutumia umeme aliouzalisha kutoka kwenye maporomoko ya maji.

Ubunifu huo umeendelea kutajwa kama ishara ya uwezo wa wabunifu wa ndani kutengeneza suluhisho kwa changamoto zinazozikabili jamii.

Ngailo anasema anatamani kuona vipaji na mawazo ya wabunifu mbalimbali nchini vikitambuliwa na kupewa nafasi ya kukua ili kuchangia maendeleo ya jamii.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *