Mkandarasi anayejenga mradi wa njia ya umeme wa Kilovoti 220 kati ya Songea mkoani Rvuma hadi Masasi mkoani Lindi ametahadharishwa juu ya kuchukuliwa hatua za kisheria kutokana na kuchelewesha kazi hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo, Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi ameonesha kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa
mradi huo.
Msikilize hapa.
Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Songea kupitia Tunduru hadi Masasi unatekelezwa na Mkandarasi Kalpataru Power kutoka India.
Mradi huo unatarajiwa kuiunganisha Mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye Gridi ya Taifa pamoja na kuimarisha upatikanaji wa umeme katika Wilaya ya Tunduru na maeneo jirani.
Mhariri @moseskwindi
(Feed generated with FetchRSS)