Pwani. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amewataka wananchi kuulinda muungano na si jambo ambalo linapaswa kuchezewa ambao unatakiwa hivyo unapaswa kulindwa na kila mmoja maana ndio alama kubwa ya Tanzania.

Masauni ameyasema hayo leo Julai 22, 2026 wilayani Bagamoyo mkoani Pwani katika ziara yake ya kikazi akieleza kufurahishwa na shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Pwani zinazofanyika ambazo zinaunganisha na Zanzibar ikiwemo bandari.

“Fursa ya Muungano inatakiwa kusaidia pande zote bara na Zanzibar na katika hili itakuwa inasaidia zaidi kwenye sekta ya utalii kwani mtalii anapokuja Zanzibar anaunganisha na Bagamoyo kwenye hifadhi ya Saadani,” amesema.

Kadhalika amewataka vijana kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii katika kipindi hiki cha utandawazi kutokana na kuwepo kwa upotoshaji mkubwa unaofanywa na baadhi ya vijana.

Amewataka kutumia mitandao ya kijamii kwa mambo ambayo yatakuwa na faida kwao hususani kujifunza mbinu za kuboresha shughuli zao za kibiashara za kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake Mbunge wa Chalinze ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete amesema Chalinzi inabadilika kwa kasi kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Serikali pamoja na wananchi wa eneo hilo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete akielezea jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni aliyoifanya Chalinze mkoani Pwani, Julai 22, 2026.

Ameongeza kuwa ushirikiano baina ya viongozi na wananchi imesaidia kufanya kimbilio kwa wawekezaji wengi kutokana na kuwepo kwa miundombinu Rafiki jambo ambalo limeifanya Chalinze kukua kukua kila siku.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema Wilaya ya Bagamoyo ni kati ya maeneo ya utalii ambayo kwasasa yanakuwa kwa kasi kwa kuwa na wawekezaji wengi wazawa na wageni wanaofika kuwekeza.

“Kuhusu suala la Muungano hapa Pwani watu wengi wanakutana na kufanya shighuli mbalimbali kutoka Zanzibar na Bagamoyo ni moja ya mji ambao wananchi wananufaika na Muungano wa nchi yetu,”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *