Baraza la Madiwani Halmashauri ya mji kasulu limefanya kikao Cha kujadili hoja mbali mbali ikiwa ni pamoja na udhibiti wa mapato ambapo mgeni rasmi katika kikao hicho alikuwa ni mkuu wa mkoa wa Kigoma Barozi Saimon Sirro.

Katika kikao hicho Balozi Sirro amewatataka madiwani wa kata katika halmashauri ya Kasulu mji kusimamia kwa weledi suala la ulinzi na usalama katika maeneo Yao ili kuepuka matukio ya kihalifu yatokanayo uhamiaji haramu.

” Tuna majirani zetu ambao wamekuwa na desturi ya kuingia nchini bila kufuata utaratibu, kama tukiruhusu hali ya namna hiyo tutashindwa kusimamia suala la Usalama katika maeneo yetu , nchi ni yakwetu hivyo lazima wafuate sheria na taratibu zilizopo”

Aidha Balozi Saimon Sirro ametoa wito kwa mamlaka zote zinazosimamia masuala ya ulinzi na usalama wilaya ya Kasulu na kigoma kwa ujumla wake ikiwa ni pamoja na idara ya uhamiaji ili kuhakikisha wanafanya misako ya mara kwa mara, ili kuwabaini wahamiaji haramu.

Mbali na suala hilo la Ulinzi na usalama mkuu huyo wa mkoa amewataka madiwani katika Halmashauri ya mji kasulu kuwa waadilifu katika utendaji kazi wao pamoja na kutoa elimu juu madhara ya uhamiaji haramu kwani wameaminiwa na kuchaguliwa na wananchi ili waweze kuwaletea maendeleo ikiwemo usimamizi wa miradi na kuhakikisha usalama katika maeneo Yao .

Baraza Hilo la Madiwani ni la Robo ya pili ya mwaka, ambapo limefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji kasulu mkoni Kigoma.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *