Serikali imesema inaendelea kufanya tathmini kuhusu tamko la Jumuiya ya Madola lililotolewa Julai 10 mwaka huu, lililoitaka Tanzania kuchukua hatua ndani ya muda maalumu kuhusu kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa ametoa kauli hiyo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi katika Soko la Machinga na Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Msigwa amesema Serikali inalifanyia kazi suala hilo na itatoa mwelekeo wake baada ya kukamilisha tathmini hiyo.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *