Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Chaani Visiwani Zanzibar imesema imefanikiwa kufanya uwekezaji wa zaidi ya Shilingi Milioni 417 katika sekta mbalimbali za miradi ya maendeleo ikiwemo huduma za kijamii.
Akitoa taarifa ya uwekezaji huo, Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed amesema fedha hizo zimetokana na ushirikiano wa Ofisi ya Mbunge na wahisani.
Miongoni mwa sekta zilizonufaika kwa uwekezaji huo ni elimu, uwezeshaji wananchi kiuchumi, afya, kilimo, usafiri na usafirishaji, habari na mawasiliano na maji safi na salama.
Mhariri @moseskwindi
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)