Shambulio la wanajihadi wa kiislamu wenye uhusiano na mtandao wa Al Qaeda wakishirikiana na waasi wa Tuareg kaskazini mwa Mali ambalo lilisababisha vifo vya askari zaidi ya 50 wa Bamako na mamluki wa Urusi, linatoa sura mpya ya mzozo wa nchi hiyo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi ya kushtukiza ya Julai 18 kulenga msafara wa wanajeshi wa Mali waliokuwa wanatoka mji wa Anefis, yameonesha namna makundi hayo yenye silaha yanaendelea kuimarika yakiibua maswali kuhusu ufanisi wa mkakati wa jeshi la Mali hasa baada ya kupata msaada zaidi toka Urusi.

Licha ya kuwa makundi haya mawili yamekuwa na malengo tofauti kwa muda mrefu, hivi karibuni yameongeza ushirikiano wao hasa kutokana na kile wanaamini adui yao ni mmoja na nijeshi la Mali na washirika wake.

Kuongezeka kwa mashambulizi ya waasi, kunakuja miaka kadhaa kupita tangu Mali isitishe utekelezaji wa mkataba wa amani wa mwaka 2015 uliotiwa saini Algeria, kisha baadae kuondoka kwa walinda amani wa umoja wa Mataifa MINUSMA, Bamako ikigeukia kupata msaada toka kwa Urusi.

Wachambuzi wa mambo wanasema ushirikiano wa wanajihadi wa kiislamu Pamoja na makundi mengine yenye silaha nchini Mali, huenda kukachochea ushirikiano kama huo kwenye mataifa mengine ya ukanda wa Sahel, hatua ambayo huenda ikafanya kuwa ngumu zaidi kwa nchi hizo kudhibiti kuenea kwa uasi kwenye nchi zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *