
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Judith Suminwa, anatembelea maeneo yanayosumbuliwa na maambukizi ya Ebola aina ya Bundibugyo, ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya Elfu moja kwa mujibu wa Shirika la afya duniani WHO.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Siku ya Alhamisi, Waziri Mkuu Suminwa, aliwasili Kisangani, na sasa anatarajiwa kuzuru Bunia, Mongbwalu na Rwampara yaliyoathiriwa zaidi na Ebola Mashariki mwa DRC.
Suminwa anakuwa kiongozi wa juu kutembelea maeneo yaliyoathiriwa, licha ya Waziri wa afya, Roger Kamba kutembelea mara tatu maeneo yaliyoathiriwa, kuwahakikishia wenyeji kuwa, serikali jijini Kinshasa, haijawasahau.
Akiwa Kisangani, Suminwa amesema serikali ya DRC tayari imetoa Dola Milioni 50 ili kusaidia kupambana na maambukizi ya Ebola, huku wahisani wakitoa Dola nyingine Bilioni 1 kusaidia katika mapambano hayo.
Jean Bosco Kisoke, kiongozi wa mashirika ya kiraia kutoka mkoani Ituri, amesema ziara hizi zinazofanywa na wakuu wa serikali ni muhimu, lakini raia wa kawaida, wanahisi kuwa, hakuna mipango ya makusudi inayofanyika ili kumaliza maambukizo hayo kwa haraka.