Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema serikali itazingatia masuala ya kitaalamu, ushauri wa kisayansi na tafiti katika kuendeleza sekta za mifugo na uvuvi.

Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amebainisha hayo (22.01.2026), alipofanya ziara ya kikazi katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo Mkoani Morogoro, ili kuweka pamoja makubaliano ya kushirikiana kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi na SUA.

Akizungumza na baadhi ya wanachuo, wakati akijionea shughuli mbalimbali zinazofanywa chuoni hapo, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza kuzingatia masuala ya kitaalamu, ushauri wa kisayansi na tafiti katika kuendeleza sekta za mifugo na uvuvi.

“Wizara imepewa maelekezo ya Mhe. Rais pamoja na Dira ya Maendeleo ya miaka 25 inatuelekeza kutoka kufuga kienyeji na kufuga kisasa pamoja na kufuga kwa tija na ufanisi.” Amefafanua Mhe. Balozi Dkt. Bashiru

Aidha, ameongeza kuwa SUA ni moja ya vyuo vyenye heshima nchini katika masuala ya mafunzo, ushauri wa kitaalamu na masuala ya utafiti kwenye kilimo, mifugo, uvuvi na misitu.
#startvupdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *