Matokeo ya awali yanaonyesha chama hicho cha Kansela Friedrich Merz kinatarajiwa kujizolea asilimia 33.3 ya kura kikifuatiwa na chama cha siasa za wastani zinazoegemea mrengo wa kushoto cha SPD kikiwa na asilimia 22.1 ya kura.

Chama kinachofuata siasa kali za mrengo wa kulia, AfD, kilichokuwa kinafuatiliwa kwa karibu na waagalizi wa uchaguzi huu kinatazamiwa kupata asilimia 14.5 ya kura.

Vyama vingine ikiwemo kile cha kijani (Die GrĂ¼nne) na FDP vinatarajiwa kupata matokeo mabaya.

Uchaguzi wa jimbo la NRW, ambao ni wa kwanza tangu Merz alipoingia madarakani mwezi Mei, unaangaliwa kama kipimo kwa serikali yake ya muungano. Kansela huyo alisema atafuatilia matokeo ya uchaguzi huu kwa makini kujua kile wapiga kura wanachokitaka katika siasa za kikanda na kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *