#HABARI: Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Chrispin Chalamila amesema katika kipindi cha Julai hadi Disemba mwaka jana, wameweza kuokoa shilingi bilioni 60.2 kutokana na kudhibiti vitendo vya rushwa huku kati ya kesi 489 za rushwa zilizofikishwa Mahakamani katika kipindi kifupi Jamhuri ikishinda kwa asilimia 68.8.

Waziri Mkuu Dkt Mwigulu Lameck Nchemba amepongeza mafanikio hayo akisema ni kazi nzuri ambayo Watanzania wanatamani kusikia na kwamba hata Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliagiza tuhuma za rushwa kuhakikishwa zinafikishwa mamlaka sahihi, zinachunguzwa mara moja, uchunguzi unakamilika na mashauri yanafikishwa Mahakamani ili haki itendeke.

Akasema fedha zilizookolewa na TAKUKURU zimetumika kwa afua zingine za maendeleo ikiwemo afya ya mama na mtoto, vifaa tiba, miundombinu na maendeleo mengine.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *