#HABARI: Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, amesema nafasi za kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa kujitolea Haziuzwi, zinatolewa bure kwa kila kijana wa Kitanzania mwenye sifa zilizoainishwa na JKT.

Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo Ofisini kwake Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma, wakati walipokuwa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari waliotaka kufahamu zaidi namna JKT linavyotekeleza jukumu la Malezi ya Vijana na umuhimu wake kwa Taifa.

Amefafanua kuwa nafasi zote zimepelekwa katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani, hivyo amewataka wananchi kuepuka matapeli watakaotaka kiasi chochote cha fedha ili kuwapatia vijana wao nafasi hizo.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *