#HABARI: Wajasiriamali jijini Mbeya wameutaka uongozi wa jiji kuunda Tume maalum ya kuwachunguza na kuwaondoa watendaji wa mitaa, kata, na watumishi wa jiji wanaotuhumiwa kuomba rushwa katika mchakato wa mikopo ya asilimia 10.

Malalamiko hayo yameibuka kutokana na madai kuwa baadhi ya watumishi wasio waadilifu hutengeneza vikundi vyao binafsi au kutoa mikopo kwa watu wasio na sifa kwa maslahi yao, jambo linalokwamisha walengwa halisi kupata mitaji.

Hoja hizo zimetolewa wakati wa mkutano kati ya wajasiriamali na uongozi wa jiji uliolenga kujadili changamoto za kibiashara na kutafuta mbinu za kufikia masoko ya Kimataifa.

Wajasiriamali hao wamesisitiza kuwa kuondolewa kwa mianya ya rushwa na watumishi wasio waaminifu ni hatua muhimu itakayosaidia kukuza biashara zao na kuhakikisha fedha za serikali zinatumika kama ilivyokusudiwa kwa maendeleo ya jamii.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *