#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Alhaji Abubakar Kunenge, ametoa ufafanuzi kuhusu mgogoro wa ardhi wa hekari 850 katika Kijiji cha Lupunga, wilayani Kibaha, kufuatia malalamiko ya wakazi kudaiwa kuvamia eneo la mwekezaji.

Katika maelezo yake, Alhaji Kunenge amebainisha mmiliki halali wa eneo hilo ili kumaliza sintofahamu iliyokuwepo na kuhakikisha usalama wa ardhi unazingatiwa kwa mujibu wa sheria.

Pamoja na ufafanuzi huo, Mkuu wa Mkoa amewahimiza wananchi wa Pwani kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upandaji miti litakalofanyika Januari 27 mwaka huu. Zoezi hilo litaenda sambamba na ugawaji wa miche ya mikorosho zaidi ya milioni moja kwa wakulima, lengo likiwa ni kuimarisha mazingira na kukuza uchumi wa wakazi wa mkoa huo kupitia zao la korosho.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *