Katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, siku hii imepewa mwelekeo wa vitendo kwa kusisitiza upandaji wa miti kama ishara ya kuthamini na kulinda mazingira.

Kufuatia ushauri huo, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeungana na Watanzania wengine kuadhimisha siku hiyo kwa kupanda mti, tendo linalobeba ujumbe wa mazingira ni utu na maendeleo endelevu. Tukio hilo limeongozwa na Ephraim Mafuru, ambapo mti wa matunda umepandwa kuashiria ukuaji na mafanikio yanayoendelea kushuhudiwa katika sekta ya utalii.

Hatua hiyo inaonesha dhamira ya sekta ya utalii katika kulinda mazingira sambamba na kukuza uchumi, huku ikiweka msingi imara wa urithi chanya kwa vizazi vijavyo.

#MazingiranaUtu #Tanzaniaunforgettable
#StaeTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *