#HABARI: Umoja wa Madereva Bodaboda jijini Dar es Salaam umejitokeza kushiriki zoezi la upandaji miti, katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea mafanikio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika siku yake ya kuzaliwa.

Akizungumza kwa niaba ya umoja huo wakati wa zoezi hilo, Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva Bodaboda Saidi Nchime, amesema kuwa wameamua kushiriki shughuli hiyo kama ishara ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika kulinda amani, umoja na mshikamano wa Watanzania.

Amesema zoezi la upandaji miti lina lengo la kuhamasisha utunzaji wa mazingira pamoja na kuendeleza maono ya maendeleo endelevu, huku pia wakikata keki maalum kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia katika siku yake ya kuzaliwa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *