
Jeshi la Sudan limeeleza kuwa limevunja mzingiro wa karibu miaka miwili wa wanamgambo wa RSF katika mji muhimu katika mkoa wa Kordofan, na kudhibiti njia kuu za usafirishaji.
Taarifa ya Jeshi la Sudan imesema kuwa limefungua njia inayoelekea katika mji wa Dilling huko Kordofan Kusini.
Taarifa hiyo imesema:” Wanajeshi wetu wamemsababisha adui hasara kubwa za kinyenzo na kuua na kujeruhi wanamgambo wa RSF.
Wanamgambo wa RSF hadi sasa hawajatoa taarifa yoyote ya kuthibitisha au kukanusha kauli hiyo ya jeshi la Sudan.
Jeshi la Sudan linapigana na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kwa karibu miaka mitatu sasa.
Dilling iko katikati ya Kadugli – makao makuu ya jimbo lililozingirwa na el-Obeid, makao makuu ya jimbo jirani la Kordofan Kaskazini.
Hali ya kibinadamu katika mji wa Dilling huwenda ikaboreka kwani jeshi la Sudan sasa litaweza kupeleka huko suhulal za kitiba, chakula na bidhaa nyingine za kibiashara ambazo zilizuiwa kuingia katika mji huo baada ya kuzingirwa na wanamgambo wa RSF.
Baada ya kufurishwa katika mji mkuu, Khartoum mwezi Machi, wanamgambo wa RSF walielekeza huko Kordofan na katika mji wa El-Fasher, ambao ulikuwa ngome ya mwisho ya jeshi la Sudan huko Darfur.
Ripoti za mauaji ya halaiki, ubakaji, utekaji nyara na uporaji ziliibuka baada ya wanamgambo wa RSF kuudhibiti mji wa El Fasher. Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imeanzisha uchunguzi rasmi wa “uhalifu wa kivita” wa pande zote mbili zinazohusika vitani huko Sudan.