#HABARI: Zaidi ya kaya 2,000 zenye uhitaji mkoani Manyara zinatarajiwa kunufaika na msaada wa chakula kutoka taasisi ya Mati Foundation, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kampuni ya Mati Super Brands Ltd kurejesha faida kwa jamii inayozunguka kiwanda chake.

Tayari awamu ya kwanza ya msaada huo imewafikia wakazi wa kaya 37 katika kata ya Bagara, wilayani Babati, ambapo Meneja Mradi Isack Piganio amebainisha kuwa lengo kuu ni kusaidia makundi yaliyo katika mazingira magumu na wenye mahitaji maalum ili kuwapunguzia ugumu wa maisha.

Zoezi hilo limepokelewa kwa furaha na wanufaika pamoja na viongozi wa serikali walioipongeza kampuni hiyo kwa kuwakumbuka watu wenye uhitaji na kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto za kijamii.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *