Mwanamume wa Kijapani mwenye umri wa miaka 51 aliyeibiwa huko Hong Kong ni miongoni mwa wale wanaoaminika kushambuliwa katika jaribio la wizi kwenye eneo la kuegesha magari la Uwanja wa Ndege wa Haneda jijini Tokyo Januari 30 kabla ya kuondoka kwenda Hong Kong.

Mapema Januari 30, polisi nchini Japani walisema kwamba wanaume wanne walishambulia kundi la watu wanne kwenye maegesho ya magari. Walisema tukio hilo lilitokea karibu na gari lililokuwa limebeba pesa taslimu zenye thamani ya takriban yeni milioni 190, au karibu dola milioni 1.2, lakini pesa hizo hazikuibwa.

Polisi walisema Januari 29 usiku, saa kadhaa kabla ya shambulio hilo, watu watatu walishambulia kundi la raia wa Japani na China kwa kinyunyizio kama cha pilipili barabarani katika Kata ya Taito. Walisema washambuliaji hao walitoroka na masanduku yenye pesa taslimu zenye thamani ya yeni zaidi ya milioni 400, au dola zaidi ya milioni 2.58.

Polisi walisema wahusika katika visa vyote viwili walikimbia kwa gari. Wanatafuta wahusika hao, ambao inaaminika bado wako nchini Japani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *