Mchambuzi wa siasa za kimataifa, Dkt. Richard Mbunda, amesema utawala wa kijeshi wa sasa nchini Burkina Faso unaoongozwa na Ibrahim Traoré umekuwa na tija kwa wananchi kutokana na kujikita katika matumizi ya rasilimali zilizopo kwa ajili ya kuleta maendeleo ya nchi, ikiwemo kuboresha miundombinu.
Ameongeza kuwa kwa kawaida tawala za kijeshi huonekana kudhoofisha maendeleo ya nchi kutokana na changamoto za uwajibikaji, lakini hali imekuwa tofauti chini ya utawala wa Traoré nchini Burkina Faso.
✍Halima Addallah
Mhariri | John Mbalamwezi
#AzamTVUpdates