Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Simiyu, imemhukumu Kabote Magembe (23), mkazi wa Mkula wilayani Busega, kifungo cha miaka minne jela kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Tukio hilo limetokea Septemba 11, 2025, katika eneo la Mgodi wa Ikinabushu wilayani Bariadi.

Inaelezwa kuwa mshitakiwa alikuwa akigombana na Mawilo Masalu (35), ndipo alimchoma kisu mgongoni, hali iliyosababisha kifo chake kutokana na kupoteza damu nyingi.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *