Chanzo cha picha, Getty Images
Muda wa kusoma: Dakika 4
Bei ya Bitcoin imeporomoka kwa kiwango kisicho na kifani katika muda wa miezi 15, licha ya Rais wa Marekani Donald Trump kuIunga mkono hadharani sarafu hiyo fiche ya kidijitali.
Bei ya Bitcoin moja ni $66,000 (kama £48,700), kiwango ambacho ni cha chini zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu mwezi Oktoba 2024 ikiashiria kushuka kwa asilimia 24 tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Thamani ya sarafu hiyo ilipanda kwa kiwango kikubwa huku bei yake ikiongezeka na kufikia takriban dola 122,200 Oktoba.
Kujihusisha kwa Trump katika sekta hiyo na uungaji mkono wake wa wazi wa sarafu hiyo kulichoche imani ya wawekezaji, hasa wakati rais huyo wa Marekani alipoahidi kurahisisha sheria zinazoongoza uwekezaji wa kidijitali.
Moja wapo wa hatua za kwanza ambazo Trump alichukua aliporejea Ikulu ya White House mnamo Januari 2025 ilikuwa kutoa agizo kuu lililolenga kuifanya Marekani kuwa “kituo kikuu cha sarafu ya kidijitali duniani.”
Katika mwaka wake wa kwanza madarakani, Trump alizindua sarafu yake ya kidijitali, iliyopatia kampuni zake faida kubwa. Pia aliendelea kujihusisha na World Liberty Financial, shirika lingine la uwekezaji wa sarafu ya kidijitali inayomilikiwa na familia ya Trump.
Katika utawala wake wa sasa Trump, ameidhinisha sheria ya serikali kuu kutoa usaidizi wa kwa uwekezaji wa kidijitali, kufurusha maafisa wa dara ya Haki iliyozingatia utekelezaji wa sheria ya sarafu ya kidijitali, nayo Tume ya Usalama na ubadilishanaji wa fedha ikiachana na shughuli ya utekelezaji na uchunguzi unaohusiana na sarafu hiyo.
Mnamo Novemba, Wabunge wa cha cha Democratic katika Kamati ya inayoshughulikia masuala ya sheria walikosoa “ajenda ya kuunga mkono sarafu ya kidijitali” ya Trump, ikibainisha kuwa rais alikuwa amekusanya zaidi ya dola bilioni 11 za mali ya sarafu hizo na kupata dola milioni 800 za mapato ya kibinafsi kutoka kwa mikataba ya sarafu-fiche tangu aingie madarakani.
Kufuatia msukosuko wa soko la sarafu hiyo siku ya Alhamisi bei ya Bitcoin zimeshuka kwa 32% katika muda wa miezi 12 iliyopita, kuelekea viwango vilivyoonekana mara ya mwisho mapema 2024 na 2021.
Bitcoin, inayojulikana zaidi ulimwenguni, ni aina ya sarafu ya kidijitali ambayo haidhibitiwi na taasisi kuu ya kifedha.
Kwa nini Bitcoin imepoteza thamani yake?
Bei ya Bitcoin inapanda na kushuka kwa kasi ya ajabu, lakini wachambuzi katika Benki ya Deutsche walisema katika Jumatano kwamba kushuka kwa bei yake hivi majuzi “kulisababishwa na” uteuzi wa Trump wa Kevin Warsh kama mwenyekiti mpya wa Hifadhi ya kitaifa ya Marekani.
Baadhi wanaamini Warsh itatumia mbinu “ngumu” zaidi, kuweka viwango vya riba vya juu, wakati sera ya fedha inayoweza kunyumbulika zaidi inaelekea kusaidia uwekezaji katika mali kama vile sarafu za kidijitali.
Deutsche Bank ilibainisha kuwa bei ya Bitcoin imekuwa ikishuka kwa muda wa miezi minne, huku hisia hasi kuhusu sarafu hiyo ikiongezeka.
Alisema: “Hali hii ya wawekezaji kuendelea kuuza, kwa mtazamo wetu, inaonyesha kuwa wawekezaji wa jadi wanapoteza imani, kutokana na ukosoaji wake ambao unazidi kuongezeka kila uchao.”
Ingawa Benki ya Deutsche haitarajii crypocurrency kutoweka, haioni thamani ya Bitcoin ikifikia viwango vya juu chini ya utawala wa Trump.
Benki hiyo ilisema kuwa sarafu ya kidijitali inabadilika kutoka kuwa “mali ya kubahatisha” n akuwa kama rasilimali ambayo “inahitaji kupata jukumu lake mahususi.”
William Barheidet, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya uwekezaji ya cryptocurrency Abra Capital Management, anaunga mkono kwamba soko la sarafu hiyo linapevuka, lakini anatabiri kuimarika kwa bei.
Alisema: “Sitegemei litapanda haraka, lakini sioni kwanini haliwezi kuimarika,” akihoji kuwa hii sio mara ya kwanza kwa Bitcoin kushuhudia mabadiliko makubwa.
Aliongeza: “Njia pekee ambayo itafanya hali kuwa mbaya ni ikiwa tutaingia vitani kwa njia moja au nyingine.”
Huku hayo yakijiri, bei ya sarafu mbili maarufu za kidijitali, Ethereum na Solana, imeshuka kwa karibu asilimia 37 tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Kulingana na CoinGeco, taasisi ambayo inafuatilia utendaji wa maelfu ya sarafu hizo za kisiri, soko lake lilipoteza zaidi ya dola trilioni moja katika thamani yeke mwezi uliopita pekee, na jumla ya dola trilioni mbili ya thamani yake mnamo mwezi Oktoba mwaka jana.
Stifel, kampuni ya uwekezaji na utafiti iliyo na makao yake nchini Marekani, ilisema katika barua kwa wawekezaji kwamba bei za Bitcoin zinaweza kushuka hadi $38,000. Kampuni hiyo ilitaja mwelekeo mpya wa sarafu hiyo kuongezeka kwa uwiano kati ya mienendo ya sarafu hiyo ya kidijitali na dola ya Marekani.
Wiki iliyopita, thamani ya dola ilishuka hadi kiwango cha chini kabisa katika miaka minne.
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi