Serikali imesaini mikataba mitano inayolenga kuwawezesha vijana kupata ajira nje ya nchi, huku mikataba mingine 16 ikiwa katika hatua za mwisho za kukamilika.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amesaini makubaliano hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa kipindi cha Imbeju Bongo Fursa na jarida la Mapitio ya Vijana.
Katika hafla hiyo, amewahimiza wadau mbalimbali kuwazingatia vijana wabunifu kutoka NEDC ili kuwaendeleza na kukuza bunifu zao.
#AzamTVUpdates
Mhariri | @rajjmsangi