Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), anayeshughulikia afya, Dkt. Jafar Seif, ameagiza kuhakikisha shughuli ya ulipaji fidia kwa kwa nyumba nane zitakazopisha ujenzi wa kituo cha afya katika Kata ya Buguruni jijini Dar es Salaam inaharakishwa ili kuondoa vikwazo vinavyoweza kuchelewesha utekelezaji wa mradi huo.
Dkt. Seif amelitoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kimkakati katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambapo ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, Meya wa Jiji Nurdin Bilal na Mkurugenzi wa Jiji Elihuruma Mabelya.
#AzamTVUpdates
✍Upendo Michael
Mhariri | @rajjmsangi