Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri amesema kuwa, Cairo inaunga mkono umoja wa ardhi ya Somalia na inasisitiza umuhimu wa ushiriki wake katika misheni ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika nchini humo.

Rais wa Misri amesema hayo katika mazungumzo yake mjini Cairo na mgeni wake Rais Hassan Sheikh Mahmoud wa Somalia.

Marais hao mbali na kujadili masuala ya pande mbili wamezunguumzia matukio ya hivi karibuni yya kieneo na kimataifa hususan hatua ya hivi karibuni ya utawala haramu wa Israel ya kutangaza kutambua jimbo lililojitenga na Somalia la Somaliland kama nchi huru uamuzi ambao umeendelea kukosolewa na kulaaniwa kimataifa.

Rais wa Misri amebainisha kuwa, “Misri inapinga vikali hatua yoyote inayohatarisha usalama na utulivu wa Somalia na eneo la Pembe ya Afrika.”

Amesisitiza kwamba Misri itaendelea na juhudi zake za kudumisha usalama na utulivu nchini Somalia, Pembe ya Afrika, na Bahari Nyekundu.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, hatua ya hivi karibuni ya utawala haramu wa Israel ya kutangaza kutambua jimbo lililojitenga na Somalia la Somaliland kama nchi huru uamuzi ambao umeendelea kukosolewa na kulaaniwa kimataifa.

Jumuiya mbalimbali za kieneo kama EAC, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC na mataifa ya kikanda yameungana na walimwengu kupinga vikali hatua hiyo ya Israel yakisisitiza imekiuka kanuni na sharia za kimataifa.

Somaliland ilijitenga na Somalia mwaka 1991 kufuatia vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe lakini haijawahi kutambuliwa rasmi na nchi yoyote mwanachama wa Umoja wa Mataifa. Jamhuri hiyo iliyotangaza kujitenga na Somalia imeanzisha sarafu yake, bendera na bunge, ingawa maeneo yake ya mashariki yameathiriwa na mzozo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *