Ikiwa leo ni siku ya kwanza tangu kuzinduliwa kwa Soko la Kariakoo na Rais Samia Suluhu Hassan, wafanyabiashara wamekuwa na hekaheka za kujipanga kuingia na kufanya shughuli zao. Katika hatua hiyo, wamevutiwa na mazingira rafiki ya kufanya biashara.
Wakizungumza na Azam News walipokuwa katika vizimba vyao, wafanyabiashara hao wametoa ushauri kwa wenzao kufanya shughuli zao ndani ya soko badala ya kukaa nje.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi