Sherehe na maandamano ya kuadhimisha miaka 47 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yatafanyika katika miji zaidi ya 1,400 nchini kote, huku waandishi wa habari wa ndani na nje wapatao 7,700 wakitarajiwa kuripoti matukio hayo.

Kamal Khodadadeh, afisa katika Baraza la Uratibu wa Uenezaji wa Kiislamu, ametangaza katika mkutano na waandishi wa habari leo Jumanne kwamba waandishi hao wa vyombo vya habari wataripoti matukio ya maandamano na sherehe hizo za kitaifa zinazofanyika kila mwaka kwenye maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ambayo kwa kawaida hufanyika Februari 11.

“Mwaka huu, waandishi wa vyombo vya habari vya kigeni na wapiga picha wapatao 200, na kwa jumla zaidi ya waandishi habari 7,700 wa vyombo vya habari vya ndani na kimataifa, wataripoti sherehe za Bahman 22 kote nchini”, amesema Kamal Khodadadeh.

Ameongeza kuwa: “Zaidi ya hayo, chaneli zote za Shirika la Utangazaji la Iran (IRIB), ikiwa ni pamoja na timu za habari zaidi ya 350, vitengo vyote vya matangazo ya kimataifa … pamoja na chaneli zote ya mikoa … zitaripoti habari za moja kwa moja na kusambaza picha za sherehe hizo.”

Hata hivyo, ameongeza kwamba “hatupaswi kusahau kwamba tunaomboleza damu ya karibu mashahidi 2,400 na karibu majeruhi 3,000 hapa nchini. “Adui alitaka kutumia vibaya maandamano ya amani kwa ajili ya kuvunja mshikamano wa wananchi, kwa sababu wakati wa Vita vya Siku 12 (mnamo Juni mwaka jana), umoja usio na kifani na mshikamano mtakatifu iliibuka nchini,” Kamal Khodadadeh.

Mamlaka za Iran zimethibitisha kwamba mashirika ya ujasusi ya Marekani na Israel yalihusika moja kwa moja katika machafukko hayo, yakitoa ufadhili, mafunzo na msaada wa vyombo vya habari kwa wahusika. 

Sherehe za tarehe 22 Bahman (11 Februari) zinaadhimisha kupinduliwa utawala wa kidikteta wa Pahlavi, ambao ulikuwa ukiungwa mkono kikamilifu na kusaidiwa na Marekani, katika majira ya baridi kali ya 1979.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *