#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, ametoa onyo kali kwa baadhi ya viongozi wa vijiji na kata katika Wilaya ya Kiteto wanaotuhumiwa kuchochea migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
Akizungumza katika kikao kazi kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa lengo la kuwajengea uwezo madiwani juu ya sheria na maadili ya uongozi, Sendiga amesisitiza kuwa Serikali haitavumilia viongozi wanaosababisha uvunjifu wa amani na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ili kukomesha mivutano hiyo.
Kwa upande wao, madiwani wa Kiteto wakiongozwa na Hamza Ally wa Kata ya Dosi Dosi pamoja na Abdallah Bundala wa Kata ya Songambele, wameahidi kuwa watatuzi wa migogoro badala ya kuwa sehemu ya tatizo ili kuimarisha usalama wa wananchi.
Mwezeshaji kutoka TAMISEMI, Yustina Bubinza, ameongeza kuwa mafunzo hayo ni muhimu katika kuwakumbusha viongozi wajibu wao wa kisheria na kimaadili, hatua itakayosaidia kuleta uwajibikaji na kudumisha mshikamano kati ya jamii zinazozunguka wilaya hiyo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
(Feed generated with FetchRSS)