#INTERTAINMENTUPDATE
Bad Bunny alipanda jukwaani kwenye Super Bowl LX 2026 kwa onyesho la halftime ambalo liliibua mijadala mikubwa duniani kote. Wengine waliliona kama hatua ya kihistoria kwa muziki wa Kilatini, huku wengine wakilibeza vikali wakidai halikuwa “show ya kiwango cha Super Bowl.” Miongoni mwa waliokosoa kwa sauti kubwa walikuwa mastaa na watu mashuhuri kama Donald Trump na Chris Brown, ambao walihoji ubora na burudani ya onyesho hilo.
Hata hivyo, kelele za wakosoaji hazikuendana na takwimu za watazamaji. Licha ya kubezwa, onyesho la Bad Bunny lilivutia zaidi ya watazamaji milioni 128, na kulifanya kuwa miongoni mwa halftime shows zilizotazamwa zaidi katika historia ya Super Bowl. Hii ilionyesha wazi kuwa mitazamo ya mitandaoni na reality ya viewership ni vitu viwili tofauti kabisa.
Mwisho wa siku, Bad Bunny alifanikiwa kuweka alama yake kwenye moja ya majukwaa makubwa zaidi ya burudani duniani. Onyesho lake lilithibitisha kwamba hata unapokutana na ukosoaji mkubwa hata kutoka kwa watu maarufu bado unaweza kufanya matokeo makubwa na kuacha historia yako mwenyewe.
✍️✍️ @future_designer

(Feed generated with FetchRSS)