Benki ya Equity Tanzania imeweka lengo la kukusanya shilingi bilioni 200 kupitia akaunti mpya ya akiba ya muda maalum iitwayo Wezesha Akaunti, fedha zitakazotumika kuongeza uwezo wa benki kutoa mikopo, hususan kwa wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa (MSMEs), pamoja na kuimarisha vyanzo vyake vya ufadhili.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa wakati wa uzinduzi uliofanyika leo Februari 11, 2026 jijini Dar es Salaam, njia ya kukusanya fedha hizo ni kupitia wateja kufungua akaunti ya akiba ya muda maalum, ambapo mteja huweka fedha kwa muda wa miaka mitatu, kwa kiwango cha chini cha shilingi 500,000.

Akaunti hiyo inatoa riba ya asilimia 13 kwa mwaka, huku mwenye akaunti akiruhusiwa kutumia hadi asilimia 80 ya thamani ya amana yake kama dhamana ya mkopo bila kuvunja uwekezaji wake. Hatua hiyo inalenga kuongeza mzunguko wa mikopo, bila kupunguza akiba iliyokusanywa na benki.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa benki hiyo, Theresia Aloyce Mayanie amesema fedha zitakazokusanywa zinatarajiwa kusaidia upanuzi wa mikopo kwa wateja wa biashara, sambamba na kuongeza uwezo wa benki kufadhili miradi ya uzalishaji.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *