Mmiliki wa kampuni ya Matondo Breweries Investment Limited, Matondo Kilugala Malanda iliyopo wilayani Bukombe, amefikishwa katika Mahakama Kuu ya Mkoa wa Geita kujibu mashtaka manane ikiwamo kugushi stampu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Matondo amesomewa mashitaka yake mbele Hakimu Mkazi wa Mahakama Kuu Geita, Cleofas Waane Februari 10, 2026 ambapo shauri lake limeanza kusikilizwa rasmi.
Wakili wa Serikali, Emmanuel Cheneko amedai kuwa mtuhumiwa huyo anakabiliwa na tuhuma nane za kikodi, ikiwamo kuanza uzalishaji bila kuwa na leseni halali na matumizi ya stempu bandia.
Tuhuma nyingine ni kukutwa na bidhaa zinazopaswa kulipiwa ushuru wa bidhaa bila kulipiwa ushuru huo, pamoja na kushindwa kuandaa na kuwasilisha ritani za ushuru wa bidhaa kama inavyotakiwa kisheria.
Aidha, Meneja wa Idara ya Upelelezi wa Kodi Kanda ya Ziwa, Joel Mbilinyi, amewakumbusha wazalishaji wa vinywaji changamshi kuwa pamoja na kupata usajili kutoka BRELA, wanapaswa pia kupata leseni ya uzalishaji kutoka TRA kwa mujibu wa sheria, ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria.
Amewaraka wasambazaji na walaji kuomba risiti za EFD wanaponunua bidhaa na kuhakiki stamp kwa kutumia programu ya hakiki stamp hali itakayosaidia kutokupotea kwa mapato, kulinda afya za walaji na kuleta usawa katika ushindani sokoni.
#StarTvUpdate
(Feed generated with FetchRSS)