Madrid, Hispania. Real Madrid na UEFA zimetangaza kuwa zimefikia rasmi hatma ya  mgogoro wao wa kisheria kuhusu pendekezo la kuanzishwa kwa Ligi ya European Super League.

 Mabingwa hao wa Hispania walikuwa ndio klabu pekee iliyobakia katika mpango huo, baada ya Barcelona kujiondoa wiki iliyopita.

Klabu hiyo ya Hispania ilikuwa timu ya mwisho kusalia kwenye mpango huo baada ya majirani zao Barcelona kujiondoa wiki iliyopita.

Katika taarifa ya pamoja kutoka UEFA, Real Madrid na Shirikisho la Klabu za Soka Ulaya, ilielezwa:

“UEFA, Umoja wa Klabu za Soka barani Ulaya na Real Madrid tumefikia makubaliano kwa maslahi ya soka la  Ulaya. Makubaliano haya ya kimsingi pia yatasaidia kumaliza migogoro inayohusiana na European Super League. Baada ya miezi kadhaa.

Klabu za Ligi Kuu ya England,  Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Tottenham Hotspur zote zilihusika katika pendekezo la awali la Super League na zilijiunga mwaka 2021. Hata hivyo, upinzani mkali kutoka kwa mashabiki wao ulizilazimu klabu zote sita kujiondoa ndani ya saa 72.

Barcelona ilichukua muda na kubakia katika mpango huo hadi wiki iliyopita ilipoamua kujiondoa huku rais wa Barcelona ambaye aliweka wazi kwamba wamejiondoa kwa sababu wanahitaji kuendelea kuweka mahusiano mazuri na UEFA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *