#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameingilia kati na kutatua mgogoro wa ardhi katika eneo la Nyakasangwe, Kinondoni.
Hatua hiyo imekuja baada ya mwanamke mmoja, aliyetambulika kwa jina la Glory Munisi, kutoa malalamiko ya kutapeliwa fedha zake wakati akijaribu kununua kiwanja katika eneo hilo.
Baada ya kusikiliza pande zote mbili, RC Chalamila ametoa milioni tano na kumrejeshea Bi. Munisi na kutoa agizo kwa Mwenyekiti wa mtaa wa eneo husika kurejesha fedha hizo kwake kabla ya siku ya kesho February 14, 2026 kumalizika.
Uamuzi huo umelenga kumpatia haki mwananchi huyo ambaye alikuwa ameshaingia hasara kutokana na udanganyifu uliofanyika.
RC Chalamila amewaonya viongozi wa mitaa kutenda haki na kusimamia uadilifu katika masuala ya ardhi.
Pia, amewasihi wananchi kuwa makini na kufuata taratibu zote za kisheria wanaponunua viwanja ili kujiepusha na mitego ya matapeli.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.