Mwakilishi wa kudumu wa Israel katika Umoja wa Mataifa Danny Danon amesema kuwa suluhu ya mataifa mawili si jambo linalowezekana kwa Israel. Danon ametoa kauli hiyo kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa ngazi ya juu wa kimataifa wa usuluhishi wa amani kuhusu suala la Palestina na utekelezaji wa suluhisho la mataifa mawili, unaosimamiwa na Ufaransa na Saudi Arabiakatika siku ya ufunguzi ya mkutano maalum wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA.

“Viongozi wengi leo watazungumza mustakabali wa baadae wakati Hamas haitakuwa sehemu ya Gaza, lakini nitawauliza, ni nani atafanya hivyo? Nani atahakikisha kuwa Hamas sio sehemu ya Gaza? Israel imejitolea kuendeleza vita hivi hadi tuwarejeshe mateka wote, hadi Hamas watakapoangamizwa. Huo ndio wakati ambao tunaweza kuzungumza juu ya mustakabali wa baadae.”Matamshi ya mwanadiplomasia huyo yanatolewa wakati mataifa kadhaa ikiwemo Ufaransayakiendelea kutangaza kulitambua taifa la Palestina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *