Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya haki za binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu amesema, analengwa na hujuma za kumchafulia jina na kumtaja kwa ubaya kwa sababu ya kulaani vita vya utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza na Ukingo wa Magharibi.

Pamoja na hayo, Albanese ameieleza Al Jazeera Mubashara kwamba, hujuma na mashinikizo yanayotolewa dhidi yake si chochote yakilinganishwa na yale wanayokabiliana nayo Wapalestina.

Amefafanua kwamba, amekuwa akiandamawa na hujuma za kumchafulia jina na kumtaja kwa ubaya kwa sababu ya kulaani vita vya utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza na Ukingo wa Magharibi. Ripota huyo maalumu wa UN ameongeza kuwa hujuma hizo dhidi yake zimeshtadi baada ya kuchapishwa ripoti zake kuhusu ukiukwaji wa haki za Wapalestina.

Albanese ametoa wito pia kwa nchi Magharibi wa kuzitaka zichunguze na kujadili ripoti zilizowasilishwa kuhusu ukiukwaji huo, badala ya kumuandama yeye na kumshinikiza.

Kwa mara nyingine tena Ripota huyo Maalumu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya haki za binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu amesisitizia udharura wa kuuwajibisha utawala wa kizayuni kwa ukiukaji wa haki za binadamu pamoja na kuwalinda raia wa Palestina.

Inafaa kuashiria kwamba Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot ametoa tuhuma za uongo dhidi ya Albanese na kumtaka ajiuzulu kutokana na kuukosoa utawala wa Kizayuni na kulaani mauaji ya kimbari Wapalestina uliyofanya huko Ghaza…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *