#HABARI: Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, inaendelea leo Jumatatu Februari 16, 2026 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam. Kesi hiyo ipo mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Dunstan Ndunguru, ambapo shahidi wa saba anatarajiwa kuanza kutoa ushahidi kuanzia saa tatu kamili asubuhi.

Katika usikilizwaji wa Ijumaa iliyopita, mashahidi wawili walitoa ushahidi, akiwemo shahidi anayelindwa P6(24), dereva bodaboda anayejitambulisha pia kama mwanachama wa CHADEMA, pamoja na askari mpelelezi H.3923 Koplo Michael (36) mkazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro.

Shahidi P6 alidai mahakamani kuwa alishawishiwa na Lissu kuhamasisha vurugu na kuzuia uchaguzi, huku Koplo Michael akieleza namna walivyomkamata kijana mmoja mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kuhamasisha vurugu kabla ya kuachiwa kwa dhamana na baadaye kuitwa kutoa maelezo kama shahidi katika kesi hiyo.

Miongoni mwa hoja zilizobishaniwa mahakamani ni tofauti za maelezo kati ya ushahidi unaotolewa na mashahidi mahakamani na taarifa walizorekodi awali kwa polisi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *