Kwa miongo kadhaa, kumekuwapo mjadala mpana miongoni mwa wanasayansi kuhusu chimbuko la mwanadamu.

Baadhi wamekuwa wakitetea nadharia ya mageuzi wakieleza kuwa mwanadamu anatokana na mabadiliko ya viumbe kama sokwe, huku wengine wakisisitiza mtazamo wa uumbaji kwamba mwanadamu ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.

Katika muktadha huo, wanasayansi vijana kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Chuo Kikuu cha Theofilo Kisanji wameandaa kongamano la kitaaluma kujadili nadharia ya Intelligent Design, wakirejea tafiti na ushahidi wa kisayansi unaochochea mjadala huo.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *