#HABARI: Serikali imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 70 kupitia tozo na ada mbalimbali kutokana na utekelezaji wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amebainisha kuwa kiwango hicho kinatarajiwa kupanda na kufikia shilingi trilioni 2.3 punde mradi utakapoanza kazi rasmi, huku utekelezaji wake ukiwa tayari umefikia asilimia 81 na unatarajiwa kukamilika Julai 2026.
Mradi huu wa kimkakati wenye thamani ya dola bilioni 5.649 umetoa manufaa makubwa ya kiuchumi kwa wazawa, ikiwemo kuzalisha ajira 10,000 ambapo asilimia 75 zimeshikiliwa na Watanzania.
Aidha, zaidi ya kampuni 200 za ndani zimepata zabuni zenye thamani ya shilingi trilioni 1.325, hatua inayochochea ukuaji wa biashara za ndani na kuimarisha uwezo wa kampuni za kitanzania katika miradi mikubwa ya Kimataifa.
Mhe. Salome amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake uliowezesha uboreshaji wa miundombinu mbalimbali, ikiwemo barabara zenye urefu wa kilomita 304 kando ya mradi huo.
Uwekezaji huu si tu umerahisisha ujenzi wa bomba hilo lenye urefu wa kilomita 1,443, bali pia umechochea uchumi wa wananchi wa maeneo husika na kuimarisha hadhi ya Tanzania katika sekta ya nishati duniani.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.