#HABARI: Takribani nyumba 10 za wakazi wa Mtaa wa Miwale, Kata ya Pangani mkoani Pwani, zimebomolewa na watu wanaodaiwa kuwa ni wamiliki wa eneo hilo, jambo lililowaacha wananchi hao bila makazi na katika simanzi nzito.
Waathirika wa tukio hilo wamelalamika kuwa zoezi hilo limefanyika kwa kushtukiza bila kupewa taarifa yoyote ya awali, hali iliyosababisha upotevu na uharibifu mkubwa wa mali zao huku wakiiomba Serikali kuingilia kati ili kupata haki na msaada.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Bw. Nickson Simon, ameeleza kufuatilia suala hilo kwa ukaribu baada ya kupokea malalamiko hayo kwa njia ya simu, huku uongozi wa Serikali ya Mtaa ukijaribu kutoa ufafanuzi juu ya kiini cha mgogoro huo.
Licha ya jitihada za kuwapata viongozi wa mtaa ofisini kugonga mwamba, Mwenyekiti wa mtaa huo, Bw. Amosi Mkwawa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limeibua hofu na masikitiko makubwa miongoni mwa majirani na wakazi wa eneo la Miwale.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.