#HABARI: Mashahidi wa kificho wawili wa upande wa Jamhuri ambao wamejitambulisha kama wafuasi wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), wametoa ushahidi wao katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ambaye anashtakiwa kwa mashtaka ya kosa la uhaini.
Mashahidi hao ni wa saba aliyepewa jina la siri kama (P2) ambaye ni fundi umeme, mkazi wa Songea mkoani Ruvuma ni shahidi wa nane ni (P8) ambaye ni Mfanyabiashara wa matunda soko la Manyema, akiwa mkazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
Wawili hao waliongozwa na wakili Mkuu wa Serikali, Ignas Mwinuka na Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga, ambapo wametoa ushahidi wao kwa nyakati tofauti mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru.
Shahidi huyo wa saba ambaye ni mfuasi wa CHADEMA tangu 2021, amedai kuwa alimuona Bwana Lissu akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari akitoa maelezo kwamba hakutakuwa na uchaguzi wa Oktoba 2025 na wanaotaka kugombea Ubunge na Udiwani wasahau.
Shahidi huyo aliyekuwa ndani ya chumba maalum alidai kuwa Lissu alisisitiza namna ya kuzuia uchaguzi mkuu usifanyike ili kuleta mabadiliko, akihamasisha kila mmoja awe jasiri.
Alipoulizwa na wakili Mwinuka nini kiliendelea amedai kuwa alimfuata kiongozi wake wa Baraza la Vijana na baada ya kufanya mawasiliano Aprili 7, 2025, waliambiwa mkutano utafanyika Ruvuma Aprili 10, 2025 na watoa mchango kwa njia ya tone tone.
Aidha shahidi huyo amedai kuwa ilipofika Aprili 9, 2025 akiwa katika shughuli zake alifuatilia pia taarifa za habari aliona kwamba Tundu Lissu, amekamatwa na licha ya Lissu kukamatwa, ilipofika Aprili 10, 2025 alijiandaa na kwenda kwenye mkutano huo uliofanyika Ruvuma ambapo alikuta magari ya Polisi ambao walisema hakutakuwa na mkutano.
Zaidi www.itv.co.tz
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania