#HABARI: Waganga wa jadi katika Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora wameeleza kusononeshwa na kitendo cha kutotambulika rasmi kwenye matukio mbalimbali ya kitaifa, licha ya mchango wao mkubwa katika jamii.

Mwenyekiti wa waganga hao aliwasilisha kilio hicho mbele ya Katibu wa NEC, Itikadi, Mafunzo na Uenezi wa CCM, Ndg. Kenani Kihongosi, wakati wa ziara ya viongozi hao mkoani Tabora ya kukagua uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi.

Akijibu ombi hilo katika mkutano wa hadhara, Katibu wa Uenezi, Kenani Kihongosi, aliwahakikishia waganga hao kuwa Serikali na Chama Cha Mapinduzi vinatambua na kuthamini umuhimu wao katika utamaduni na ustawi wa jamii.

Katika kuonyesha utambuzi huo kwa vitendo, Kihongosi aliwakaribisha viongozi wa waganga hao kuketi katika meza kuu ya viongozi, hatua iliyopokelewa kwa furaha kama ishara ya heshima na ushirikishwaji wa kundi hilo katika shughuli za kiserikali na kisiasa.

‎Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *