Mradi wa Israel wa kilimo na makazi wa ekari 520 huko Solai, Kaunti ya Nakuru nchini Kenya umezua mjadala mkali wa kitaifa. Wakenya wametumia mitandao ya kijamii kupinga mradi huo, wanaotaja kuwa mwanzo wa unyakuzi wa ardhi za nchi hiyo na utawala ghasibu wa Israel.

Pamoja na kuwa mwekezaji wa Israel wa mradi huo wa kilimo cha vitalu, Erez Rivkin ameahidi kilimo cha kisasa kitakachowafaa Wakenya, lakini aghalabu ya wananchi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki wametilia shaka malengo halisi ya mradi huo.

Wasiwasi mkubwa wa Wakenya juu ya mradi huo umetokana na historia ya uporaji wa ardhi za Palestina, na mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

Mtumiaji mmoja wa mtandao wa kijamii wa X kwa jina la Kipruto Too amesema, Wakenya hawapasi kufanya kuwa wa kawaida suala la kuishi pamoja na Waisraeli. Mfano mzuri ambao Wakenya wanaweza kupata somo la kihistoria ni mauaji ya kimbari ya Gaza huko Palestina.

Mwanamitandao mashuhuri wa Kenya kwa jina la Raptcha The Sayantist ameandika: Unakubali vipi kuiuzia Israel ardhi ya Kenya, wakati ambapo dunia nzima inawafukuza Waisraeli katika ardhi zao? Kenya kwa hakika inalifedhehesha bara Afrika. Lazima tusimame na kuwafurusha wauajai hao wa umati kabla ya mambo kuharibika.

Mkenya mwingine kwa jina Black Kosgei amesema, “Binafsi nawaogopa Waisrael hata kuliko magaidi wa al-Shabaab, hao watu hawana uzuri hata kidogo.”

Kadhalika Wakenya wametilia shaka muda wa ununuzi wa kipande hicho cha ardhi, hasa baada ya janga la bwawa la Solai la 2018, ambalo liliua watu wengi na familia zikazopoteza makazi, ingawaje ‘uchunguzi rasmi’ ulihusisha janga hilo na mvua kubwa na miundombinu dhaifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *