#HABARI: Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, kufuatia kifo cha nguli wa muziki na mtunzi wa wimbo, ‘Tanzania Yetu’, Mzee Steven Hiza.
Rais Dkt.Samia amesema “Tunatambua na tutaendelea kuenzi mchango wake mkubwa katika sekta ya muziki, ambapo wimbo wake wa Tanzania Yetu umeipamba nchi yetu, umetukumbusha wajibu wetu kwa Taifa letu, umetuelimisha na kutuburudisha kwa takribani miaka 60 sasa”
Rais Samia amewaombea subra na uvumilivu familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu, Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania