Wataalamu wa lishe wanasema kula maharage mara kwa mara kunaweza kukusaidia kupunguza uzito kwa njia ya afya.
Wanadai kuwa maharage yana nyuzinyuzi nyingi zinazokufanya ushibe muda mrefu (bye bye kula kila saa 😅) na protini inayosaidia kujenga misuli na kuchoma mafuta.
Tofauti na vyakula vya kukaanga na vyenye sukari nyingi, maharage husaidia kudhibiti sukari kwenye damu na kupunguza tamaa ya kula kupita kiasi.
👉 Jaribu kula maharage mara 3-4 kwa wiki
👉 Yapike kwa kuchemsha au kwa mafuta kidogo
👉 Yaambatanishe na mboga za majani au nafaka zisizokobolewa
👉 Kunywa maji ya kutosha + ongeza mazoezi ya mara kwa mara
Kumbuka… hakuna miujiza ya siku moja… ni nidhamu na maamuzi sahihi kila siku. 💪🌱
Je, wewe unapenda kula maharage kwa mtindo gani? Maharage ya nazi, ya kupika tu, au ya kuchanganya na wali? 🍛
Andika kwenye comments 👇, ‘msanue’ na jirani yako!
#AzamTVUpdates
✍John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)