Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka, amesema baadhi ya watumishi wasiokuwa waaminifu wamekuwa wakihujumu mifumo ya kisasa ya kidigitali kwa lengo la kuendelea kunufaika na mifumo ya zamani inayodaiwa kukosa ufanisi na kuchochea ubadhirifu wa mali za umma.
Amesema licha ya juhudi kubwa za serikali kuimarisha sekta ya TEHAMA kupitia uanzishaji wa mifumo ya kidigitali, bado kuna upinzani wa ndani unaochelewesha mageuzi hayo.
Balozi Kusiluka ametoa kauli hiyo jijini Arusha wakati akifungua Mkutano wa Sita wa Serikali Mtandao uliowakutanisha zaidi ya washiriki 1,400 kutoka taasisi za umma na binafsi kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kuimarisha matumizi ya teknolojia katika utoaji huduma.
Alisisitiza kuwa serikali haitavumilia vitendo vya kuhujumu mifumo ya kidigitali, akibainisha kuwa mageuzi ya teknolojia yanalenga kuongeza uwazi, ufanisi na kupunguza mianya ya ubadhirifu katika taasisi za umma.
✍ Ramadhani Mvungi
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)