#HABARI: Vikundi 19 vya mamalishe, wajasiriamali, na maafisa usafirishaji katika Kata ya Gongolamboto jijini Dar es Salaam, vinatarajiwa kunufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.

Diwani wa kata hiyo, Wakili Kenneth Mlawa, amewataka wanufaika kutumia fedha hizo kwa tija ili kukuza biashara zao, akisisitiza kuwa hatua hiyo inaendana na dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kila Mtanzania anafikia maisha bora kupitia shughuli za uzalishaji.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo wa Kata, Khadija Omary, amewakumbusha waombaji umuhimu wa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kuruhusu makundi mengine yenye uhitaji kunufaika na mzunguko wa fedha hizo.

Baadhi ya walengwa, wakiongozwa na Emmanuel Magoma na Sarah Kenedy, wameishukuru serikali kwa fursa hiyo na kueleza kuwa elimu waliyoipata juu ya matumizi sahihi ya mikopo itawasaidia kuendesha biashara zao kwa ufanisi zaidi na kuleta mabadiliko ya kweli katika kaya zao.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Powered by #MCHEZOSUPA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *